top of page

NEWS WITH UCA TZ

Pata habari mbali mbali kuhusiana na Mziki na Sanaa na UCA Tz.

Project ilianza tarehe 05/08/2013  ndani ya  Genious Records.

Kazi nzuri ilifanywa na Genious Records kwa kuanza kutengeneza sample beat zaidi ya 3 hadi kufikia uchaguzi wa official beat iliyotumika kwenye wimbo huu. Genious Records ni studio inayofanya kazi zake chini ya usimamizi wa Producer Mode. Studio inazaidi ya miaka 2 kazini na imeshafanya kazi na wasanii mbalimbali underground na well known artist. Inapatikana maeneo ya Kigogo Njiapanda, jijini Dar-es-Salaam.

 

Utengenezaji wa UCA Tz Anthem umechukua wiki takribani 3 kukamilika; hii ni kuhakikisha tunatoa kitu kizuri chenye kukubalika kwa jamii. UCA Tz Anthem Part 1, ni nyimbo inayoelezea dhumuni la Project UCA Tz , pia inahamasisha vijana waamke na kujikabili na changamoto zinazowakatisha tamaa kwa kile wanachokifanya. Nyimbo imeshirikisha 7 young talented upcoming artists.

 

Katika kuhakikisha UCA Tz Anthem inakamilika vizuri ndani ya wiki 3 za utayarishaji, kuna vikwazo vingi vilivyojitokeza kuanzia umeme hadi upatikanaji wa wasanii sahihi tunaowahitaji but UCA Tz team haikurudi nyuma na kufanya kazi yao.

UCA Anthem -The Making.

REGISTER KUWA MEMBER WA UCA TZ

FORMALITIES

  • Tuma details zako kwenye kwa no. 0684546900. Details zako zikielezea information kama inavoonekana kwenye document yetu hapo chini.

  • Lipia registration fee kupitia no. yetu 0684546900

  • Usahili utakamilika baada ya siku 3 

  • Baada ya wiki 2 utapata UCA Tz ID Card itakayokutambulisha kama mwanachama wa UCA Tz


FAIDA ZA UWANACHAMA

  • Unapata kitambulisho cha UCA Tz

  • Punguzo la asilimia flani katika shughuli za UCA Tz

  • Kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za UCA Tz kwa kuzingatia vigezo na masharti ya UCA Tz

  • Nafasi ya kushare mawazo yako kuhusiana na mziki na sanaa na changamoto za vijana kwa ujumla

  • Wigo wa kukutana na kujuana na watu wenye chachu ya maendeleo ya vijana, kimziki na sanaa

Check out the Official UCA Tz Anthem on YouTube

Hatimae ile nyimbo iliyokuwa ikingojewa kwa hamu imetoka. UCA Tz Anthem imefanyika Genious Records ikiwa imeshirikisha wasanii vijana 7. Iangalie hapa.

bottom of page